MAKUBWA HAYA..!! MSANII AFA AKITAJA JINA MAINDA


MSANII aliyefariki dunia hivi karibuni mjini Morogoro, Sherry Magali, anadaiwa kuwa alikuwa akilitaja jina la Ruth Suka ‘Mainda’ kila mara hadi alipofikwa na umauti.
Marehemu Sherry Magali enzi za uhai wake.
Chanzo chetu makini kilichokuwa karibu na msanii huyo wa filamu, kinasema Sherry alianza kugoma kula akidai hadi amuone msanii mwenzake huyo ambaye alikuwa jijini Dar es Salaam anakoishi.
 
Msanii wa 'Bongo Movie' Ruth Suka (Mainda) akiwa katika pozi.

Mpashaji huyo alisema hata siku aliyofariki pia alilitaja jina hilo, kitendo kilichowaumiza sana baadhi ya ndugu na marafiki. Mainda ambaye alikuwa ni rafiki wa marehemu, alikiri kusikia jambo hilo na anasikitika kwamba siku aliyopanga kwenda, ndiyo ambayo mwenzake alifariki.

0 comments: