SIMBA KAMA KAWA SARE TENA
SIMBA
SC imetoa sare ya sita mfululizo tangu kuanza kwa Ligi Kuu ya Vodacom
Tanzania Bara, baada ya kufungana bao 1-1 na Mtibwa Sugar, Uwanja wa
Jamhuri, Morogoro jioni ya leo.
Ushindi huo, unawafanya Mtibwa wafikishe pointi 14 kileleni mwa ligi hiyo, wakati Simba SC imefikisha pointi 6 leo
Simba SC ilikwenda kupumzika ikiwa
tayari inaongoza kwa bao 1-0, lililotiwa kimiani na beki wa kimataifa wa
Uganda, Joseph Owino dakika ya 35 kwa kichwa akimalizia mpira wa adhabu
uliopigwa na Emmanuel Okwi.
Hali hiyo iliwafanya vinara wa hao wa
Ligi Kuu wapate bao la kusawazisha dakika ya 58, mfungaji Mussa Hassan
Mgosi aliyetumia makosa ya beki wa kulia, William Lucian ‘Gallas’
kuchanganyana na kipa wake, Manyika Jr.
Mtibwa Sugar: Said
Mohammed, Hassan Ramadhani, David Luhende, Andrew Vincent, Salim
Mbonde, Shaaban Nditi, Mussa Ngosi, Mohamed Ibrahim, Ame Ally, Mussa
Nampaka na Ally Shomary.
Simba SC: Peter Manyika, William Lucian ‘Gallas’, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’, Hassan Isihaka, Joseph Owino, Jonas Mkude, Ramadhani Singano ‘Messi’, Awadh Juma, Elias Maguri/Amisi Tambwe dk76, Said Ndemla na Emmanuel Okwi/Uhuru Suleiman dk75.

0 comments: