YANGA YAPEWA KICHAPO NA KAGERA SUGAR

BAO pekee la kiungo Paul Ngway, dakika ya 52 jioni ya leo limeipa Kagera
Sugar ushindi wa 1-0 dhidi ya Yanga SC, Uwanja wa Kaitaba, Bukoba katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
Yanga SC ilimaliza mchezo huo pungufu, baada ya Nahodha wake, Nadir Haroub ‘Cannavaro’ kutolewa kwa kadi nyekundu dakika ya 80 na refa Abdallah Kambuzi wa Shinyanga, baada ya kumpiga kichwa Rashid Mandawa wa Kagera.
Baada ya mchezo huo, mashabiki wa Yanga SC walimtisha refa kiasi cha kutolewa uwanjani kwa msaada wa askari wa Polisi.
 
Kagera Sugar: Agathon Anthony, Benjamin Asukile, Abubakar Mtiro, Erick Kyaruzi, George Kavilla, Babu Ally, Julius Ambrose, Paul Maona, Rashid Mandawa, Atupele Green na Adam Kingwande.
Yanga SC: Deo Munishi ‘Dida’, Juma Abdul, Oscar Joshua, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Kevin Yondan, Mbuyu Twite, Hassan Dilunga, Haruna Niyonzima, Genilson Santos ‘Jaja’, Mrisho Ngassa na Andrey Coutinho.

0 comments: