AIBU:MWESHIMIWA MBOEWE AFANYA MAMBO YA AIBU MBELE YA WATOTO ALA DENDA NA MKE WAKE UKU AKIPIGWA PICHA

Kiongozi wa Kambi ya Upinzani (Bungeni), Freeman Mbowe, wiki iliyopita alipamba vilivyo mitandao ya kijamii, haikuwa kwa sababu ya tishio la maandamano kuhusu Daftari la Kudumu la Wapiga Kura wala Katiba Mpya, ‘topiki’ ilikaa kimapenzi zaidi.
Kiongozi wa Kambi ya Upinzani (Bungeni), Freeman Mbowe akimkumbatia mkewe, Dk. Lillian Mbowe.
Watu aah! Mheshimiwa Mbowe, ooh hivi, mara vile! Tathmini ya gazeti hili inaonesha kuwa asilimia kubwa wanampongeza mbunge huyo wa Hai (Chadema), kwamba ni mume mzuri na baba bora wa familia yake.
Hujanyaka topiki? Wiki iliyopita katika mitandao zilienea picha za Mbowe akiwa kwenye sherehe ya kifamilia, iliyofanyika Oktoba 12, mwaka huu kwenye Ukumbi wa Kivukoni, Serena Hotel, Dar es Salaam,  huku zikimuonesha anambusu mkewe, Dk. Lillian Mbowe kwa hisia kali za malovee.
KWA NINI PONGEZI?
Uchunguzi wa gazeti hili katika mitandao ya kijamii kupitia ‘komenti’ mbalimbali pamoja na maoni ya watu kadhaa waliohojiwa mitaani na mwandishi wetu, picha hizo zinampambanua Mbowe kama kiongozi wa kisasa ambaye anajua jinsi ya kuwajibika kifamilia.
Watoa maoni wengi, wamemfananisha Mbowe na Rais wa Marekani, Barack Obama kwamba ni mfano wa kuigwa katika viongozi wanaojali familia.“Obama kwa mkewe Michelle na wanaye Sasha na Malia, ni wazi yeye ni baba bora wa familia. Kamanda Mbowe amedhihirisha kuwa siasa hazimuweki mbali mpaka akasahau familia, nimependa sana picha hizi za Mbowe na familia yake,” alisema Julie Macklin wa Sinza, Dar es Salaam.Mh. Freeman Mbowe akishoo love kwa mkewe.
Pingu Mabula katika ukurasa wake wa Facebook, aliandika: “Nimefurahishwa sana na hii picha (inayomuonesha akimkisi mkewe, huku watoto wao watatu wakiwa wanawatazama kwa tabasamu), natamani viongozi wote wawe na mahaba ya kuridhisha kwa familia zao kama hivi.”
Mwanahawa Red-guard, aliweka picha kama ambayo Pingu aliitundika Facebook kisha akasindikiza kwa maneno: “Njia ya muongo ni fupi sana, kuna waliokuwa wanadai kamanda Mbowe na mkewe hawaelewani, mara picha haziendi, hii ni kuonesha jinsi ambavyo mtu mzima alivyotulia na mkewe.
“Unakuwa na mkeo lakini hutaki kumuonesha upendo, watoto hawaoni upendo wa wazazi wao mpaka nao wanaathirika kisaikolojia, lakini picha hii ni wazi Mbowe anajenga kitu upendo ndani ya familia, wazazi wanapendana, watoto pia watapendana tu, vilevile wakiwa na familia zao watazijenga kwa upendo pia.”
PICHA PENDWA
Pamoja na ukweli kwamba picha za Mbowe akimbusu mkewe ni nyingi lakini moja iliyovutia wengi ni ile ambayo mwenyekiti huyo wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), anambusu mkewe, huku watoto wao ‘firstborn’ Dudley, Nicole na Denis wakiwatazama kwa tabasamu.
Mh. Freeman Mbowe akimbusu mkewe huku watoto wakitabasamu
Uchunguzi umeonesha kuwa picha hiyo ndiyo iliyoongoza kwa ‘kupostiwa’ katika Mitandao ya  Kijamii ya Facebook, Twitter, Instagram na mingine, huku blogu kadhaa zikiifanya habari, vilevile ikitumwa sana katika makundi ya WhatsApp.
MCHUNGAJI HARRIS KAPIGA APONGEZA
Mchungaji wa Kanisa la Nchi ya Ahadi ambaye pia ni mhamasishaji wa masuala ya kiuchumi na familia, Harris Kapiga, aliipongeza picha hiyo na akasema hashangai kwa nini inapendwa sana na watu kutokana na ujumbe inaofikisha.
Kapiga alisema: “Ni picha bora sana kwa familia. Ipo hivi, wewe baba ukitaka uwape zawadi bora kabisa watoto wako basi mpende mama yao. Ndiyo maana katika picha hiyo watoto wanatabasamu, ni zawadi kubwa sana ambayo Mbowe amewapa kwa kuonesha jinsi anavyompenda mama yao.
“Kingine ni kwamba mwanaume amepewa mamlaka, inapotokea mume anambusu mkewe hadharani kama Mbowe alivyofanya, inaonesha jinsi ambavyo upendo wake kwa mkewe hauna shaka. Ni upendo wa dhati kabisa.
“Tafiti zinaonesha pia kuwa familia nyingi za wanasiasa huchukia siasa kwa sababu ya kukosa uwepo wa baba kwa muda mwingi. Vivyo hivyo kwa madaktari, wachungaji na kadhalika, huchukia huduma za baba zao lakini Mbowe ameonesha kuwa kiongozi mkubwa wa kisiasa hakuzuii kuwajibika ipasavyo ndani ya familia.”
Baba na Mh. Freeman Mbowe akiwa na familia yake.
MWANASAIKOLOJIA CHRIS MAUKI ANENA
Mtaalamu wa Saikolojia na Uhusiano ambaye ni Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dk. Chris Mauki, alisema kuwa picha za Mbowe akimbusu mkewe hadharani zimemuongezea thamani kijamii kwa sababu watu wanawapenda wanaume wanaobeba majukumu ya kifamilia.
“Unadhani kwa nini Obama ni kiongozi mashuhuri sana duniani na anapendwa sana na watu, ni kwa sababu ya ile tabia yake ya kuwa karibu na familia yake. Kuna watu wanampenda Obama si kwa sababu ya nguvu kubwa aliyonayo kisiasa, ni kwa sababu anajipambanua kuwa baba bora wa familia.
“Jamii kubwa sasa inakosa upendo wa wazi kutoka kwa akina baba. Akina baba wengi wanaona kumbusu mkewe hadharani na kuwa karibu na familia siyo suala lenye maana kubwa, kwa hiyo wale ambao wanayafanya hayo waziwazi huonekana mashujaa.
“Mbowe anapongezwa kwa sababu ni shujaa kwenye jamii kwa sababu alichokifanya wengi hawakifanyi. Familia nyingi zinakosa upendo na kufanya mpaka watoto kuathirika kisaokolojia, watoto wanaharibika,” alisema Dk. Mauki na kuendelea:
“Viongozi wa kisiasa wanapokuwa wanajali familia zao, inatia hamasa kubwa. Hata kama nyumbani hawajibiki vizuri kifamilia lakini kwenye jamii anapokuwa muwajibikaji na watu wanamuona, huvutia wengi na kupendwa sana.”
KAMANDA MBOWE AFAFANUA
Mbowe ambaye pia ni Mwenyekiti wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), alisema kuwa picha hizo zilipigwa siku ambayo kwa hakika alikuwa mwenye furaha sana kutokana na mambo mawili yaliyogusa familia yake.
“Kwanza mke wangu alikuwa anatimiza umri wa miaka 50 ya kuzaliwa, vilevile firstborn wetu Dudley alikuwa amemaliza shahada yake ya kwanza Chuo Kikuu cha Sussex, Uingereza, kwa mambo hayo mawili, tuliona ipo haja ya kufanya sherehe, ukizingatia watoto wetu wengine wawili Nicole na Denis walikuwa wamerejea nchini kwa sababu nao wanasoma nje ya nchi.
“Siku hiyo ya tukio ilikuwa Jumapili, tulianza kwa kwenda kanisani Azania Front tukatoa sadaka, baada ya hapo tulikwenda Serena Hotel kwenye Ukumbi wa Kivukoni ambako chakula cha mchana kilikuwa kimeandaliwa, tukajumuika na ndugu wengine pamoja na marafiki.
“Haikuwa sherehe tu kusema labda nilikurupuka kumbusu mke wangu, ilikuwa sherehe ya kifamilia, kumpongeza mke wangu na mtoto wetu,” alisema Mbowe.

0 comments: