MADHARA YA KULALA NA NGUO ZA NDANI.

Madaktari na waalamu wa afya wanashauri kulala bila nguo za ndani wakati wa usiku ili kuwezesha viungo vya uzazi kupata hewa ya kutosha ili kuepuka maambukizi ya fangasi na kutoa harufu mbaya katika sehemu za siri. Kuvaa nguo za ndani wakati wa kulala usababisha kubana sehemu za siri na joto kupita kiasi ambayo usababisha joto kupita kiasi na unyevu na kuvutia ukuaji wa fangasi na bakteria kwa jinsia zote huku pia zikisababisha upungufu wa mbegu za kiume na harufu mbaya.
Tambua kuwa joto la mwili ushuka kiasi unapolala na kukuwezesha kupata usingizi mzuri wakati wa usiku hivyo kulala na nguo za ndani au nguo zozote zinazobana ni kinyume chake na huongeza mikunjo kweneye ngozi na kupunguza uzuri wa ngozi. Ikumbukwe kuwa hii haiwausishi wanawake au wanaume wenye matatizo maalumu yanayowapaswa kuvaa nguo za ndani usiku kama hedhi kwa wanawake na matatizo ya uzazi. Hivyo ni muhimu kulala bila nguo za ndani au nguo zinazobana mwili wako ili kuepuka madhara haya.

0 comments: