MZEE CHILLO AGOMA KUZUNGUMZIA MAKUBALIANO YA UKAWA
MKONGWE katika
filamu za Bongo, Ahmed Ollutu ‘Mzee Chillo’ amefunguka kuwa yeye si
mwanasiasa hivyo hawezi kuzungumza chochote juu ya Umoja wa Katiba ya
Wananchi (Ukawa). Akijibu swali la mwandishi wetu baada ya kuulizwa
anazungumziaje kitendo cha Ukawa kusaini makubaliano ya kusimamisha
mgombea mmoja mmoja kuanzia ngazi ya serikali za mitaa mpaka uchaguzi wa urais utakaofanyika mwakani alisema:
“Mimi siyo mwanasiasa, huwa nafuatilia kujua wamezungumza nini, tena
siyo sana kisha naachana nao, niulize kuhusu sanaa, hata kama niko
usingizini nitakujibu kwa sababu ndiyo kazi yangu,’’ alisema Mzee
Chillo.
0 comments: