UPDATE YA VIDEO: CHIDI BENZ APANDISHWA KIZIMBANI KISUTU
Msanii wa Hip Hop, Rashid Makwiro ‘Chid
Benz’ leo amepandishwa kizimbani kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu
jijini Dar es Salaam na kusomewa mashitaka matatu ya kukutwa na madawa
ya kulevya, vifaa vya kutayarishia, uvutaji wa madawa, usafirishaji na
utumiaji wa madawa hayo ambayo alikamatwa nayo kwenye Uwanja wa Ndege wa
Julius Nyerere, Novemba 23, 2014.
Kesi hiyo imeahirishwa hadi Novemba 11
mwaka huu na msanii huyo ametupwa rumande kwa kukosa wadhamini. Hata
hivyo, atarudishwa kesho kukamilisha taratibu za dhamana ambapo
wadhamini wawili walitakiwa kutoa Shs. Milioni moja kama bond.
0 comments: