MZEE WA UPAKO ASAKWA, ADAIWA KUTISHA KUMUUA MUUMINI WA GWAJIMA
LILE sakata la Mchungaji
wa Kanisa la Maombezi (GRC) Ubungo – Kibangu, Dar, Lusekelo Anthon ‘Mzee
wa Upako’ kufyatua risasi mtaani limechukua sura mpya baada ya kijana
aliyejitambulisha kwa jina la Robert Lugala, mkazi wa Kibangu kuibuka
na kudai alitishiwa kuuawa kwa kupigwa risasi na mchungaji huyo.
Kijana anayejitambulisha kwa jina la Robert Lugala, anayedai kutishiwa maisha na Mchungaji Lusekelo Anthon.
Akizungumza na waandishi wetu juzi jijini Dar, Robert ambaye shughuli
zake ni kuuza chipsi usiku kucha, alisema mara kwa mara Mzee wa Upako
amekuwa akimfuata eneo lake la kazi na kumtishia maisha kwa kumwambia
maneno mbalimbali yenye vitisho.“Mara ya kwanza ilikuwa Oktoba 9, mwaka huu saa kumi kasoro usiku. Alipaki gari lake, Land Cruiser (Toyota) nyeusi. Akaniangalia na kuniambia nina macho makali. Akasema ataniombea nitaanguka. Nikamkatalia na kumwambia mimi nina nguvu za Mungu wa kweli, nasali kwa Gwajima kwa hiyo siwezi kuanguka. Aliposhindwa akaahidi kurejea siku nyingine.
“Mara ya pili ni Oktoba 13, mwaka huu saa nne usiku alikuja tena. Mara ya tatu ni Oktoba 15 saa kumi usiku akaanza kugawa pesa kwa madereva wa bodaboda huku akiwaamrisha kuniimbia nyimbo ya kunilaani. Kweli waliniimbia.
“Mara ya nne ni Oktoba 18, saa kumi usiku
alifika akawa anaongelea akiwa ndani ya gari lake na kuniuliza, ‘hivi
Robert unaringia nini? Hunijui vizuri ee?’
Mchungaji wa Kanisa la Maombezi (GRC) Ubungo – Kibangu, Dar, Lusekelo Anthon ‘Mzee wa Upako’ akizungumza jambo.
“Mara ya tano ni Oktoba 21, mwezi huu. Saa kumi usiku alikuja tena na
kupaki gari lake, akamwita mwendesha bodaboda mmoja na kumuuliza mimi
ni mtu wa wapi, sijui alijibiwa nini, akaondoka. Saa kumi na moja
akarudi tena,” anasimulia Robert.Akaendelea: “Novemba tatu, mwaka huu, saa kumi alfajiri, Mzee wa Upako alifika tena, akapaki gari lake kisha akasogea hapa na kuniambia mambo ambayo mimi sikumjibu, ndipo alipochomoa bastola yake na kufyatua risasi hewani kisha baada ya muda akapanda gari lake na kuondoka mpaka darajani.
“Hapo tayari watu walishaanza kuamka na kuja.
Mara na yeye akarudi tena na kuwaambia madereva bodaboda atakayepata ganda moja la risasi atampa shilingi elfu 50. Yalionekana maganda mawili tu.“Mimi nilikwenda kwa Afisa Mtendaji wa Mtaa wa Kibangu, Kata ya Makuburi, Amiti Msanjili nikiwa na risasi moja, nikajieleza, nikapewa barua kwenda Kituo cha Polisi Mbezi na kutoa taarifa, nikaandikisha jalada JMD/RB/11099/2014 KUTISHIA KUUA KWA RISASI ambapo sasa anasakwa na polisi.
“Nimeamua kusema haya kwa kuwa kanipa siku 30 za kuishi na muda wenyewe unaelekea kwisha, chochote kinaweza kutokea.”
MZEE WA UPAKO ALISHASEMAKatika Gazeti la Amani, toleo la juzi Alhamisi, kulikuwa na habari mbele yenye kichwa; KISA
Katika habari hiyo, mtumishi huyo aliripotiwa kutenda tukio hilo usiku wa Jumapili kuamkia Jumatatu. Alipotafutwa mwenyewe alisema:
“Ni kweli tukio hilo limetokea, ni kwamba siku ya tukio nilipofika eneo lile vijana wa kihuni walinifuata kwa nyuma wakaanza kupigapiga gari langu wengine wakizuia njia wakidai eti mimi ni Freemason.
“Nilijaribu kuwaambia mimi ni kiongozi wa kiroho ambaye namtangaza Mungu lakini badala yake wakaanza kuniangushia matusi. Ili kujiokoa nilifyatua risasi hewani kuwatayanya.”
Mzee wa Upako alisema baada ya vijana hao kutawanyika, yeye alikwenda Kituo cha Polisi Urafiki jijini Dar na kutoa taarifa.
0 comments: