WALIOPIGA KURA YA HAPANA WATISHIWA MAISHA DODOMA,,
Mmoja wa wajumbe hao, Salma Said alisema jana jioni kuwa yeye na wajumbe
wenzake wamekataa kuitikia wito wa Mwenyekiti wa Bunge, Samuel Sitta
kwenye Kamati ya Mashauriano ili kuhojiwa kuhusu kura hiyo na kutokana
na vitisho wanavyopata kutoka kwa wajumbe wenzao wameamua kuondoka
Dodoma.
Vitisho hivyo vimeripotiwa muda mfupi baada ya Sitta kuunda Kamati ya
Mashauriano ya watu tisa inayoongozwa na Makamu Mwenyekiti, Samia Suluhu
Hassan kushughulikia kura hizo zilizopigwa na wajumbe saba zinazoweka
njiapanda uwezekano wa kupatikana akidi ya kupitisha Katiba
inayopendekezwa.
Wajumbe waliopiga kura za wazi za hapana kwa ibara zote ni Adil Mohamed
Adil, Dk Alley Soud Nassor, Fatma Mohamed Hassan, Jamila Ameir Saleh,
Salma Hamoud Said, Mwanaidi Othman Twahir na Ali Omary Juma.
Kwa upande wa Tanzania Bara aliyepiga kura ya hapana kwa rasimu nzima ni
Mbunge wa Mpanda Kati (Chadema), Said Arfi na wajumbe 30 kutoka
Zanzibar wakipiga kura ya siri.
“Baada ya kupiga kura za hapana leo (jana), walijitokeza wajumbe akiwamo
(jina tunalihifadhi kwa sasa) wakaanza kutuzongazonga,” alisema Salma.
“Walituambia kuwa tumebaki hadi dakika ya mwisho halafu tunasema hapana
kwa rasimu nzima ili kula fedha za bure, wanasema bora tungeondoka na
Ukawa (Umoja wa Katiba ya Wananchi).”
Hata hivyo, alipopigiwa simu yake ya mkononi mmoja wa watuhimiwa,
alipokea na baada ya mwandishi kujitambulisha alikata simu na
alipopigiwa mara ya pili alijibu alisema; “Mimi ni mheshimiwa mwana na
niko Sudan.”
Salma alisema miongoni mwa wajumbe hao wakiwamo baadhi ya mawaziri
waliwafuata hadi nje ya ukumbi wakiwatishia kuwa watawafanyia hujuma kwa
kukataa kuunga mkono rasimu hiyo.
“Sisi tumeamua kuondoka kurudi kwetu, hatutaingia tena bungeni maana hivi vitisho vimezidi sasa,” alisema Salma.
Juhudi za kuwapata wajumbe wenzake kuzungumzia vitisho hivyo hazikuzaa
matunda, lakini Katibu wa Bunge hilo, Yahya Khamis Hamad alikiri kupokea
malalamiko hayo na kwamba amelichukulia kama suala la kisiasa.
Alisema wajumbe hao hawajasema wametishiwa kufanyiwa kitu gani, bali
walimweleza kuwa wameambiwa kuwa wamekaa pale (bungeni) kwa ajili ya
kupata pesa.
0 comments: