MAKONDA: SIKUVURUGA MKUTANO WA TAASISI YA MWALIMU NYERERE
(Patrick Bozohera na Gabriel Ng’osha/GPL)
KATIBU Mwenezi
Idara ya Hamasa na Chipukizi ya UVCCM, Paul Makonda, amekana kuhusika
katika vurugu zilizotokea jana katika mdahalo wa Katiba Iliyopendekezwa
ambao ulioandaliwa na Taasisi ya Mwalimu Nyerere chini ya Mwenyekiti
wake Joseph Butiku.
Hayo ameyasema leo katika hoteli ya Protea, Osterbay, jijini Dar es Salaam alipokutana na waandishi wa habari.
Mkutano huo ulikumbwa na vurugu wakati
aliyekuwa mwenyekiti wa kuratibu katiba mpya, Jaji Joseph Warioba,
alipokuwa akiwasilisha mada yake, katika ukumbi wa Ubungo Plaza jijini
Dar es Salaam
0 comments: