Spika wa Bunge, Anne Makinda Achaguliwa kuwa Rais Mpya wa Bunge la SADC
MKUTANO wa 36 wa Bunge la nchi wanachana wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC), umemchagua kwa kishindo Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Anne Makinda kuwa Rais wa Bunge hilo kwa kipindi cha miaka miwili ijayo.
Mbunge
wa Malawi, Njovya Lema amechaguliwa kuwa Makamu wa Rais. Makinda,
ambaye hakuwa na mpinzani katika uchaguzi huo uliofanyika juzi, aliungwa
mkono na wajumbe wote wa mkutano huo, ambao ni Maspika na Wabunge
kutoka mabunge ya nchi wanachama wa SADC.
Alichaguliwa wakati wa kuhitimisha Mkutano wa 36 wa Jukwaa la Mabunge ya SADC, uliokuwa ukifanyika mjini hapa.
Msimamizi
wa uchaguzi, ambaye ni Katibu Mkuu wa Bunge la SADC, Dk Esau Chiviya
alisema kwa mujibu wa kanuni za uchaguzi za Bunge hilo, Kanuni ya 42 (2)
inatamka wazi kuwa endapo kutakuwa na mgombea mmoja pekee, basi
atawahoji wajumbe na endapo watamkubali basi atamtangaza rasmi kuwa
amechaguliwa kushika nafasi hiyo.
“Kwa
kuwa Spika wa Bunge la Tanzania Mheshimiwa Anne Makinda hana mpinzani
na kwa kuwa nimewahoji na wote mmemuunga mkono, basi natangaza kuwa
ndiye Rais mpya wa Bunge la SADC kwa miaka miwili ijayo,” alitangaza Dk
Chiviya.
Awali,
kwa mujibu wa utaratibu wa uongozi ndani ya chombo hicho, Makinda
alitakiwa kugombea nafasi hiyo pamoja na Spika wa Ushelisheli na
Msumbiji, ambao hawakushiriki uchaguzi huo na badala yake walimuunga
mkono Makinda.
Akisoma
hotuba yake ya shukrani kwa wajumbe wa Mkutano huo, Makinda alisema:
“Ninalo deni kubwa kwenu kwa jinsi mlivyoniunga mkono na kama mnavyojua
jukumu letu kubwa mbele yetu ni kuwa na Bunge imara la SADC, jambo
ambalo nawahakikishia kwa pamoja tutafanikiwa.
habari kamili hapa
0 comments: