KAJALA, MWANAYE WAZUA GUMZO MLIMANI CITY

SEXY lady wa filamu Bongo, Kajala Masanja hivi karibuni aligeuka gumzo yeye na mwanaye walipoenda kufanya ‘shopping’ Mlimani City ambapo watu walikuwa wakiwakodolea macho kwa jinsi alivyolingana na mtoto wake.
Sexy lady wa filamu Bongo, Kajala Masanja akiwa na mwanaye Paula.
Kajala alitinga eneo hilo na mtoto wake huyo aitwaye  Paula ambapo awali walienda kupata chakula katika mgahawa wa SamakiSamaki  na kisha waliingia ndani kwa ajili ya kufanya manunuzi mengine.
“Kwa kweli Kajala amekuza maana yeye na mtoto wake wamelingana sasa na mara nyingi kwa sasa hivi wanaongozana huku wakionekana kuwa na furaha wakati wote,” alisikika mtu mmoja akizungumza.
Watoto wengine wakimkodolea binti wa kajala, Paula maeneo ya Mlimani City.
Kajala alipozungumza na  mwandishi wetu alisema kuwa hakuna kitu kinachompa furaha kama mtoto wake huyo na anapoongozana naye anazidi kufurahi zaidi.

0 comments: