MAMA KANUMBA ATOA YA MOYONI KUHUSU MWANAE SOMA HAPA
MAMA wa
aliyekuwa nguli wa filamu Bongo, marehemu Steven Kanumba, Flora Mtegoa
amesema kama kuna msanii anataka kufikia ‘levo’ za mwanaye basi asali
sana.
Akifunguka mbele ya kinasa sauti cha
Risasi Jumamosi, mama Kanumba alisema pengo la mwanaye katika sanaa
linaonekana wazi hivyo ni vyema kwa anayetaka kuliziba kufuata nyayo
zake.
”Miongoni mwa siri kubwa za mafanikio
kwa mwanangu zilizomfanya awike kuliko wengine ni kupenda kuthubutu,
kusali sana na kutokuwa na wivu wa maendeleo kwa kujiepusha na majungu.
“Tatizo wasanii wetu hawa hawapendi
kuthubutu wamekalia tu kufanyiana majungu, hawapendi kuona mwenzao
anafanikiwa wanaanza kumfitini, ni vizuri wangejifunza kitu kwa Kanumba
ambaye alipenda kuthubutu,” alisema mama Kanumba.
0 comments: