TAZAMA SAFARI YA MWISHO YA MSANII WA TMK WANAUME FAMILY, YP AZIKWA MAKABURI YA CHANG'OMBE DAR
Wasanii wa Bongo Fleva wakiuaga mwili wa marehemu Yesaya Ambikile 'YP' katika Viwanja vya TCC Chang'ombe, Dar es Salaam.
Waombolezaji wakiwa katika msiba wa msanii wa Bongo Fleva, Yesaya Ambikile 'YP' kwenye Viwanj vya TCC, Chang'ombe, Dar.
Mke wa marehemu YP, Sakina Robert (mwenye kiremba cheupe) akiwa katika hali ya majonzi.
Msanii wa Bongo Fleva, Juma Nature akizungumza jambo kwa niaba ya wasanii wenzake waliofanya kazi na marehemu enzi za uhai wake.
Baadhi ya wasanii na waombolezaji wakiwa mbele ya jeneza muda mfupi kabla ya kuuaga mwili wa marehemu.
Msanii wa filamu, William Mtitu akipita kuaga mwili wa marehemu.
Msanii wa vichekesho, Mussa Kitale 'Mkude Simba' akiaga mwili.
MSANII WA TMK WANAUME FAMILY,
Yesaya Ambikile 'YP' aliyefariki usiku wa kuamkia janai, amezikwa leo
katika makaburi ya Chang’ombe maduka mawili jijini Dar jioni hii. Baadhi
ya wasanii wa Bongo Movie waliokuwepo kuungana na wasanii wenzao wa
Bongo Fleva ni pamoja na JB, Steve Nyerere, Jacqueline Wolper, Kajala
Masanja, Shilole, William Mtitu, Mkude Simba na wengineo.
0 comments: