AMA KWELI MCHEPUKO SIYO DILI,NJEMBA ACHARANGWA MAPANGA BAADA YA KUNASWA NA MKE WA MTU
MH!
‘Haga gangi’ (haya mengine)! Simon Manase (22) ambaye ni dereva wa
bodaboda, mkazi wa Kijiji cha Nguyami, wilayani Gairo mkoani hapa
amecharangwa mapanga mwilini na kukatwa mkono wa kulia na mtu aliyetajwa
kwa jina la Frank akidai kumfumania na mkewe vichakani.
Ishu hiyo inadaiwa kujiri usiku mnene wa Oktoba 31, mwaka huu kwenye
Kijiji cha Nembo mpakani mwa Gairo na Kilosa katika muziki wa mitaani
maarufu kwa jina la ‘kigodoro’.Mwandishi wetu alipiga gia hadi kwenye
eneo la tukio na kufanikiwa kuzungumza na mashuhuda, viongozi wa kata,
Mganga Mkuu wa Hospitali ya Berega na Mkuu wa Kituo cha Polisi Dumila.
“Mkewe naye alikuwepo, alipojibu si kweli alimpiga,”alisema kijana huyo.
Juhui za mwandishi wetu kutaka kuzungumza na Frank zilikwama kufuatia mtuhumiwa huyo kutimua mbio akiogopa chombo cha habari.
Mganga mkuu wa hospitali aliyolazwa Simon, Alfred Chiponda alithibitisha kumpokea mgongwa huyo.
Mkuu wa kituo cha polisi, afande James Charles alikiri kutokea kwa tukio hilo na kusema vijana wake wanamsaka Frank.
“Siku ya tukio tulikuwa kwenye shereha ya
mwenzetu, mwanae amevunja ungo hivyo nyumbani kwake aliweka muziki wa
kigodoro, cha ajabu ilipofika saa sita usiku DJ wa muziki, Alex Munga
alitutangazia kwamba kuna watu wanapigana mapanga baada ya kufumaniana
kwenye kichaka.
“Tulikimbilia kule. Kufika tukamkuta Frank akimcharanga mapanga Simon
akidai amemfumania na mkewe ,”alisema shuhuda aliyejitambulisha kwa
jina la Elizabeth Joseph.Afisa Mtendaji wa Kijiji cha Nembo, Musa Bruno
alikiri kutokea kwa tukio hilo kwenye kijiji chake.
“Ni kweli, siku hiyo, mimi na msaidizi
wangu, Daudi Kisonela na mgambo wa kijiji tulifika eneo la tukio na
kushuhudia Simon akivuja damu mwilini huku mkono wake wa kulia
ukining’inia nusu hadi mfupa wa ndani ukionekana baada ya kupigwa
mapanga na Frank akidai kamfumania na mkewe,” alisema mtendaji huyo.
Akaendelea: “Tuliwaweka kikao, tulimhoji mke akasema mumewe alikurupuka kumcharanga mapanga mtuhumiwa kwani si kweli.
“Kwa kauli ya mama huyo tulimtia hatiani Frank, tukamkamata na
kumfikisha Kituo cha Polisi Dumila, cha ajabu wakati sisi tukitafuta
usafiri, huku nyuma mtendaji wa kata alimuachia huru Frank huku
akitukabidhi panga lenye damu kama ushahidi.”Akizungumza kwa tabu na
mwandishi wetu katika wodi ya wanaume Hospital ya Misheni ya Berega,
Gairo, Simon alisema:Akaendelea: “Tuliwaweka kikao, tulimhoji mke akasema mumewe alikurupuka kumcharanga mapanga mtuhumiwa kwani si kweli.
”Siku ya tukio nilifika kwenye kigodoro kwa
lengo la kusaka abiria, mtu mmoja aliniambia nimkodishe pikipiki
aendeshe mwenyewe, kuna watu anataka kwenda kuwafuata baada ya
makubaliano ya bei nikamkabidhi pikipiki yangu na mimi nikamsubiri
palepale.
“Ilipotimu saa 6 nikaona jamaa harudi, nikaamua kuondoka nikiamini
nitakutana naye njiani. Nilipofika mbali kidogo nikamuona Frank akiwa na
panga mkononi huku akinishutumu kwamba natembea na mkewe, nilijaribu
kubisha, akarusha panga la kichwa katika hatua ya kujihami nililipanchi
na mkono ambapo alinikata mkono.“Mkewe naye alikuwepo, alipojibu si kweli alimpiga,”alisema kijana huyo.
Juhui za mwandishi wetu kutaka kuzungumza na Frank zilikwama kufuatia mtuhumiwa huyo kutimua mbio akiogopa chombo cha habari.
Mganga mkuu wa hospitali aliyolazwa Simon, Alfred Chiponda alithibitisha kumpokea mgongwa huyo.
Mkuu wa kituo cha polisi, afande James Charles alikiri kutokea kwa tukio hilo na kusema vijana wake wanamsaka Frank.
0 comments: