HOTUBA YA SHIGONGO YAWAKUNA WAHITIMU MLIMANI SCHOOL OF PROFESSION
Mkurugenzi
Mtendaji wa Global Publishers Eric Shigongo ambaye alikuwa mgeni
rasmi
katika mahafali hayo akiongoza maandamo maalumu yaliyoandaliwa na chuo
hicho, kushoto ni Mkuu wa Chuo, Hassan Ngoma.Shigongo
akihojiwa na mwandishi wa chuo hicho cha Professional FM, Shikunzi
Haonga ambaye ni mkuu wa kitengo idara ya habari mawasiliano kwa umma
(hayupo pichani) ndani ya studio iliyopo chuoni hapo.Shigongo akikata utepe kuashiria kuzinduliwa kwa studio hiyo ya chuoni hapo. Wakijadiliana jambo kama wanavyoonekana na mkuu wa chuo hicho.Akitoa vyeti kwa wahitimu mbalimbali. Shigongo akitunukiwa diploma ya uandishi wa habari mawasiliano ya umma.Shigongo
akipigiwa Wimbo wa Taifa baada ya kutunukiwa cheti cha Uandishi wa
Habari kutokana na mchango wake mkubwa kwenye tasnia ya habari. Picha ya pamoja na wahitimu wote. Ndugu, jamaa na marafiki wa wahitimu waliofika chuoni hapo kuwapongeza.
Na Haruni Sanchawa
Wahitimu wa Chuo cha Mlimani School Of
Profession walipata msisimko mkubwa baada ya Mkurugenzi Mtendaji wa
Global Publishers, Eric Shigongo kutoa hotuba ambayo kila mmoja alijiona
kuwa anaweza kujikwamua kimaisha kama wakijibidisha katika maisha yao
ya kila siku.
Msisimko huo ulikua pale Shigongo
alipotoa simulizi ya riwaya ya ombaomba mmoja aliyekuwa akiomba kila
siku kwa kutumia kopo, kumbe kopo lile ni dhahabu yenye thamani ya
mabilioni ya fedha kwenya mahafali ya pili katika chuo hicho.
Mmoja wa wahitumu ngazi ya diploma
katika fani ya Habari na Mawasiliani ya Umma, Neema Kisimbo alimpongeza
Shigongo kuwa ni kati ya Watanzania wachache waliopewa thawabu na Mungu
hata kama akifa leo atakuwa na la kusema kuhusu alivyoweza kuisaidi
jamii.
“Baba huyu ana kipaji lakini mbali na
kipaji chake pia kujituma kwake kumefanya awe na mafanikio makubwa
maana maisha ni malengo, si kweli kwamba ameenda kwa waganga,” alisema
mhitimu huyo.
Katika mahafali hayo, Shigongo
aliwatunuku vyetu wahitimu 119 katika Chuo cha Mlimani School of
Profession Studies katika mahali yaliyofanyika katika chuo hicho hapo
jana Mbezi Kwa Msugur jijini Dar es Salaam.
Wahitumu hao walifunzu katika kozi
tofauti ndani ya chuo hicho ambapo kuna baadhi ya walipata ngazi ya
cheti na wengine katika ngazi ya diploma ambapo wote hao walitunukiwa
vyeti hivyo na mkurugenzi wa Global Publishars ambaye alikuwa mgeni
rasimi katika mahafali hayo.
Mkurugenzi huyo alitoa vyeti kwa
wahitimu 19 katika ngazi ya cheti kwa fani ya Manunuzi na Ugavi, Fani ya
Habari na Mawasiliano ya Uma wahitimu ngazi ya cheti walikuwa 20,
Rasilimali Watu wahitimu 18, ngazi ya cheti wahitimu Uhasibu walikuwa 17
, Uongozi na Biashara ngazi ya cheti sita, Mauzo na Masoko ngazi ya
cheti 3, Rasilimali Watu ngazi ya diploma sita , Uongozi wa Biashara
diploma 10, Uandishi wa habari na Mawasiliano ya Umma ngazi ya
diploma10.
Wengine ni wa Mauzo na Masoko ngazi ya diploma mmoja, Uhasibu ngazi ya diploma sita, Manunuzi na Ugavi ngazi ya diploma wanne.
Mkuu wa chuo hicho, Hassan Ngoma
alimtunuku Shigongo cheti cha Uandishi wa Habari na Mawasiliano ya Umma
ngazi ya Diploma kwa mchango wake mkubwa katika tasnia ya habari
0 comments: