WAUMINI WANAOVAA NGUO FUPI WAFUKUZWA KANISANI
Diani kusini mwa pwani ya Kenya walipigwa na
butwaa baada ya baadhi yao kuzuiwa kuingia
katika kanisa hilo kutokana na mavazi yao
yaliokuwa nusu uchi.
Julia baraza ambaye alikuwa amevalia
kisibao ,ukanda wa manjano na viatu vyenye
kisigino kirefu alishangazwa na sheria hizo mpya
ambazo zilimsababisha kukosa misa ya asaubuhi.
Kulingana na gazeti la the standard nchini
kenya,Julia alisema kuwa watu wawili
walimsimamisha nje ya mlango wa kanisa hilo na
kumwambia kwamba mtindo wake wa mavazi
ulipigwa marufuku katika kanisa hilo na kwamba
ametakiwa kuvaa mavazi ya heshima.
Aidha wasichana waliokuwa wamevalia suruali
walilazimishwa kujifunga leso juu yake.
Julia alisema kwamba iwapo makanisa yataanza
kufuata sheria kama hizo basi wengi
hawatahudhuria maombi.
Baadhi ya waumini wamesema kuwa mhubiri wa
kanisa hilo aliyejulikana kama Joseph pekee
alikuwa ametangaza katika ibada ya awali kwamba
mavazi yasio ya heshima hayatakubalika katika
kanisa hilo.
0 comments: