UKIMYA WA DIVA WA CLOUDS FM WAZUA MASWALI MENGI MITAANI, JE NI KWELI KAHAMIA EFM ?

Diva Loveness Love Maarafu Kama Divathebawse Ni Presenter Kipenzi cha wengi sana hapa Bongo Na Nje, Kutokana na Show yake ya Mambo ya Mapenzi maarufu kama Ala Za Roho Show yenye maelefu ya wasikilizaji inayokuwa inaruka mida ya usiku kupitia Clouds Fm.
Siku chache zilizopita kumekuwa na ukimwa wa presenter huyu kutosikika redioni jambo ambalo limezua maswali kwa mashabiki na wasikilizaji wake na baadhi kutengeneza hoja na maswali ya kuwa amehamia kwenye kituo kingine kipya cha redio maarufu kama Efm inayosikilizwa sana jijini Dar es salaam. Baadhi ya watu wameeneza stori hizo za kuhama na kusababisha mpaka mashabiki kuanza kusikiliza Efm wakitegemea kumsikia, jambo ambalo sio.

Kupitia social networks anazotumia Presenter huyu mashabiki wamekuwa wakicomment kuulizia nini haswa kinaendelea huku yeye akiwa kimya bila kutoa jibu lolote.

Tuna imani kuwa majibu ya ukimya huu yatapatiwa ufumbuzi na soon tutaendelea kumskia hewani kwani Diva a.k.a Divathebawse ni kipenzi cha wengi...especially vijana na watu wote wajanja.

0 comments: